33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mlinzi wa Obote arejea nyumbani baada ya miaka 50

Kampala, Uganda

Mkuu wa zamani wa Usalama wa aliyekuwa rais wa Uganda, Milton Obote, aliyedhaniwa kufa, amerejea nyumbani nchini Uganda baada ya miaka 50.

Vincent Obodo (81, ambaye aliwahi wakati mmoja kuongoza idara ya ulinzi katika ofisi ya rais, alikutana na wake zake wawili na watoto Ijumaa

Ndugu zake hawakuwahi kumuona tangu mare ya mwisho mwezi Januari mwaka 1971-wakati serikali ya Rais Obote ilipopinduliwa, mapinduzi yaliyoongozwa na Iddi Amin.

Familia na marafiki walilia machozi ya furaha wakati, Obodo aliposindikizwa nyumbani na mfanyakazi wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, Gazeti la Daily Monitor limeripoti.

Obodo ambaye alikuwa akiishi uhamishoni nchi jirani ya Tanzania kwa kipindi cha miongo mitano aliliambia gazeti la Serikali la New Vision kuwa amefurahi kurudi nyumbani.

Obote alipinduliwa na jeshi alipokuwa safarini nchini Singapore kwa ajili ya mkutano wa Jumuia ya Madola.

Obodo amesema wakati huo alikuwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta akisubiri kurudi kwa Obote kutoka Singapore ndipo alipojua kuhusu kufanyika kwa mapinduzi.

Obote alikwenda uhamishoni Tanzania, na hivyo ndivyo, Obodo alipojikuta Tanzania, na kusalia huko hata baada ya Obote kurejea tena madarakani mwaka 1980- ingawa alipinduliwa tena mwaka 1985.

Safari yake kurejea Uganda imeratibiwa kwa ushirikiano wa serikali ya Ugansa na Tanzania, afisa wa UNHCR Carol Kibuka aliliambia gazeti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles