23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Lindeni maeneo yote yenye vyanzo vyya maji- DC Moshi

Na Safina Sarwatt, Moshi

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaji Kundya, amewataka Viongozi wa Serikali za Vijiji na Kata kuhakikisha maeneo yote yenye vyanzo vya maji yanalindwa ili vyanzo hivyo viweze kuwa endelevu, huku akipiga marufuku mtu yeyote kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya eneo la mita 60 katika maeneo ya vyanzo hivyo vya maji

Kauli hiyo aliitoa Mei 10,2021 wakati alipokuwa akizindua kampeni ya upandaji miti katika eneo la mto Mombari uliopo kijiji cha Shinga, Kata ya Uru Kusini, wilayani humo zoezi ambalo liliandaliwa na Bodi ya Maji Bonde la Pangani (PBWO).

Amesema vyanzo vya maji ni lazima visimamiwe ili kukabiliana na upungufu wa raslimali maji ili yaweze kupatikana wakati wote na hivyo kutosheleza kwa sasa na upatikanaji wake uwe endelevu kwa ajili ya kizazi kijacho.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya aliwaonya watu watakaoing’oa miti ambayo imepandwa katika eneo hilo, kwani atakuwa ametangaza vita na Serikali ya awamu ya sita na kwamba itapambana naye hadi tone la mwisho.

Kwa upande wake Afisa Mazingira Ofisi ya Maji Bonde la Pangani, Mhandisi Arafa Maggidi, alisema katika kampeni hiyo ya upandaji miti imelenga kupanda miti ya aina mbalimbali katika maeneo yote ya chemichemi na mabonde ya mito yaliyopo katika mkoa huo.

“Katika Kampeni hii jumla ya miche ya miti 1,000 tumeipanda leo katika mto Mombari ambao ulikuwa umeathirika kwa kiasi kukubwa kutokana na baadhi ya wananchi kukata miti ili kupata eneo la Kilimo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles