26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mlinzi wa Dk. Slaa aendelea kuhojiwa Polisi

Dk.slaaNa Asifiwe George, Dar es Salaam
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, linaendelea kumuhoji Khalid Kagenzi ambaye ni mlinzi binafsi (PSU) wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa anayetuhumiwa kwa kosa la kutaka kumuua.
Akizungumza na MTANZANIA, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camillus Wambura, alisema wanaendelea na uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Alisema pamoja na uchunguzi huo kuendelea, lakini Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova, atalizungumzia suala hilo kesho (leo).
Kagenzi ambaye amekwa mlinzi wa Dk. Slaa katika miaka miwili, anadaiwa kutumiwa na vyombo vya usalama na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvujisha siri za chama hicho ikiwamo na kupewa kazi ya kumuua katibu huyo wa Chadema.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, alidai Kagenzi akiwa mlinzi binafsi wa Dk. Slaa katika kipindi cha miaka miwili, amebainika kutumiwa na vyombo vya usalama vya nchi pamoja na CCM kwa kuvujisha siri za chama hicho, na kupewa kazi ya kumuua katibu huyo wa Chadema.
Akielezea tukio lililombaini mlinzi huyo, Marando alidai lilitokea Ijumaa iliyopita baada ya mashushushu wa chama hicho kumwona akipanda gari lenye namba za usajili T 213 ARS linalodaiwa kutumiwa na Ofisa Usalama wa Taifa wa Kinondoni.
“Baada ya kuonekana ndipo mashushusgu wa Chadema walichukua jukumu la kumkamata na kumfanyia mahojiano ambapo walifanikiwa kumpekua katika simu zake mbili zinazotumia mitandao ya Vodacom, Airtel na Tigo.
“Katika simu hizo, walikuta ujumbe mfupi wa maneno uliokuwa ukitoka kwa …, aliyempigia mara tatu na kumtumia fedha kati ya Desemba 4, mwaka jana na Julai 14, 2014. Namba nyingine zilizokutwa zilikuwa za maofisa Usalama wa Taifa,” alisema.
Aliongeza kuwa baada ya upekuzi huo katika ‘Note book’ na simu zake, waligundua kuwa kigogo mmoja wa ngazi za juu wa CCM alimtumia muda wa maongezi wa Sh 50,000 kwa namba ya simu 0764 …222 Julai 14, 2014 na Desemba 4, 2014 alimtumia Sh 150,000.
Marando alisema katika upekuzi wa kwenye simu, walibaini mazungumzo yake yote yalikuwa yakitumia muda usiopungua saa mbili hadi tatu, na mara zote ni wakati ambao Chadema walikuwa wakifanya mikutano yao ya ndani.
“Alikuwa akitumia simu yake kurekodi kila kilichokuwa kikizungumzwa kwenye mikutano yetu na kusambaza kwa CCM, na iligundulika akiwasiliana na maofisa wa Usalama wa Taifa waliofikia 22,” alisema.
Marando aliongeza kwa kusema kuwa kama isingekuwa suala la kutolewa kwa uhai wa Dk. Slaa, wasingezungumzia suala hilo na pia anazungumziwa huenda akachaguliwa kuwa mgombea wa urais wa Ukawa.
Alisema chama hicho kimetoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili kuchukua hatua za kisheria, ambao ndio wanaweza kutaja majina ya maofisa usalama wa waliohusika na mpango huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles