22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mlinzi auawa na majambazi Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu

Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu watano wanaoudhania kuwa ni majambazi, kwa kosa la wizi na mauaji ambapo wanadaiwa kumuua Peter Ndwani (40) Masai ambaye alikuwa mlinzi.

Watuhumia hao wanadaiwa kutenda makosa hayo usiku wa kuamkia leo saa 9:00 alfajiri, baada ya kuvamia nyumbani kwa mfanyabishara wa mjini Bariadi John Sabu eneo la Kidulya halmashauri ya mji wa Bariadi lengo likiwa kuiba gunia za alzeti.

Akizungumza na waandishi wahabari leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Richard Abwao amesema kuwa watuhumiwa hao wakati wakitaka kutekeleza uharifu huo, walikutana na upinzani kutoka kwa marehemu Ndwani ambaye alikuwa mlinzi nyumbani hapo.

Alisema kuwa mlinzi wakati akipambana nao alizidiwa nguvu, na kupigwa kitu kizito kichwani na kisababisha kifo chake papohapo, na baada ya uchunguzi wa mwili wake alikutwa na majeraha kwenye paji lake la uso.

Alisema baada ya mauaji hayo watu hao walianza kutekeleza wizi huo, na wakati wakibeba magunia hayo yaliyokuwa yamehifadhiwa ndani ya ghala lililopo nyumbani hapo, ndipo mmoja wa wanafamilia alipowasikia na kupiga kelele.

“Baada ya kupiga kelele, baadhi walikimbia lakini wananchi na wanafamilia walifanikiwa kumkamata mmoja na kuanza kuwataja wenzake, ndipo na wengine wakakamatwa, ndani ya hilo ghala kulikuwemo na gunia 200 za alzeti,” amesema Abwao.

Kamanda Abwao amesema kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ikiwemo mahojiano na watuhumiwa hao waliokamatwa, na baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles