30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ally Rehmtullah kuhitimisha mafunzo kwa kufanya Onyesho la Mavazi May 22

Na Brighiter Masaki
-Dar es Salaam.

Mbunifu wa Mavazi nchini, Ally Rehmtullah, ‘AR’ kuhitimisha darasa lake la kwanza la mafunzo ya wanafunzi waliokuwa wakisomea ubunifu na uandaaji wa Mavazi kufanyika May 22, The Drum jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtanzania Digital mapema leo, Rehmtullah, amesema 1st Batch ni darasa lake la kwanza kutoka kwenye chuo chake cha mitindo, wanafunzi hao walipata mafunzo ya miezi sita na siku ya jumamosi ndio wanahitimu.

“Wanafunzi hao watahitimu mafunzo hayo kwa kufanya onyesho la Mavazi ambayo wameyabuni wao wenyewe baada ya kupata mafunzo kutoka kwa walimu tofauti tofauti.”

“Miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo ni Anjali Borkhataria, Mike Cyril Michael, Audrey Diana Harrison Matto pamoja na Ally Rehmtullah na wataonyesha nguo walizoweza kufanya kazi” amesema Rehmtullah

Aidha onyesho hilo linatarajiwa kusindikizwa na ugeni kutoka Baraza la Sanaa la Taifa, (BASATA) na (COSOTA) na watu mbalimbali kutoka katika tasnia tofauti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles