24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

MKUU WA MKOA ATAKA EKARI 3000 ZA MUHOGO

Na GUSTAPHU HAULE-PWANI


MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, amewataka wakurugenzi wa halmashauri za Kibiti, Mkuranga na Rufiji kuhakikisha wanatenga eneo la ekari 3000 kwa ajili ya kilimo cha muhogo.

Ndikilo alitoa agizo hilo juzi mjini Kibaha, wakati akizungumza na wakurugenzi hao, wenyeviti wa halmashauri na wakuu wa wilaya za mkoa huo.

Katika mkutano huo, pia alipokea ripoti kuhusu masuala ya uwekezaji kutoka timu maalumu iliyofanya ziara nchini China.

“Mahitaji ya muhogo ni makubwa nchini na hata nchi za nje na endapo zao hilo litatiliwa mkazo, linaweza kuwa zao litakaloongeza mapato ya halmashauri zetu kwa kiwango kikubwa.

“Kwa hiyo, nataka kila mkurugenzi wa halmashauri hizi tatu, aniletee mpango kazi wa kilimo cha muhogo na lazima kuhakikisha tunapata shamba la ekari 3,000 ambazo zitasaidia kuanza mchakato huo,” alisema Ndikilo.

Pamoja na hayo, Ndikilo alisema Mkoa wa Pwani unatarajia kupata wawekezaji wengi zaidi kutoka nchini China na moja ya mahitaji yao ni muhogo.

“Kwa hiyo, lazima fursa hii ikatumika kikamilifu kwa ajili ya uzalishaji ambao utaongeza kipato.

“Kuna viwanda vinavyotarajiwa kujengwa na wawekezaji hao ambavyo vitahitaji zaidi ya tani 200,000 za muhogo kwa wakati mmoja, hivyo ni vema kila halmashauri ikatambua umuhimu wa kutenga maeneo ya kilimo cha zao hilo.

“Kama kuna maeneo yaliyochukuliwa na watu siku nyingi bila kuendelezwa, ni vema wakurugenzi mkayaainisha na mniletee ofisini kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa waziri wa ardhi ili yaweze kufutwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles