23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mkutano wa Bunge kuanza leo

BungeNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUTANO wa tatu wa Bunge la 11, unaanza leo mjini Dodoma pamoja na mambo mengine, utajadili na kupitisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Bunge Dar es Salaam juzi, ilisema mjadala wa bajeti utaanza leo hadi Aprili 21.

“Baada ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kujadiliwa, Bunge litapokea na kujadili utekelezaji wa bajeti kwa wizara zote kwa mwaka wa fedha 2015/16 na makadirio ya matumizi ya Serikali kwa mwaka 2016/17, kazi ambayo itaanza Aprili 22 hadi Juni 2, mwaka huu,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, ilisema Juni 9, waziri anayehusika na mipango atawasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa nchi, ikifuatiwa na hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, kisha kufuatiwa na mjadala Juni 13 hadi 21.

“Ratiba inaonyesha kutakuwa na hati za kuwasilishwa mezani, Bunge litapokea ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2014/15  na majibu ya Serikali kuhusu hoja zitakazotolewa na mkaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, ilisema maswali 465 yataulizwa na kujibiwa na Serikali bungeni, huku kila Alhamisi yataulizwa maswali kwa Waziri Mkuu ambapo 88 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa.

“Bunge pia linatarajia kujadili na kupitisha miswada miwili ambayo ni muswada wa Sheria ya Matumizi wa mwaka 2016, kujadili na kupitisha muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2016.

“Kutakuwa pia na uchaguzi wa mwenyekiti mmoja wa Bunge ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi, baada ya Spika kufanya mabadiliko ya wajumbe wa baadhi ya kamati za kudumu za Bunge,” ilisema taarifa hiyo.

Katika mkutano huo, wabunge wapya wanne ambao ni Mbunge wa Kijitoupele (Zanzibar), Shamsi Vuai Nahodha, Mbunge wa Viti Maalumu, Ritha Kabati, Lucy Owenya na Oliver Semguruka wataapishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles