29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mkutano Mkuu FEMATA wapitisha maazimio 14 likiwamo kuanzisha benki

Na Clara Matimo, Mwanza

Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania(Femata) umepitisha maazimio 14 ikiwemo uanzishwaji wa benki ya wachimbaji wadogo wa madini na mradi wa vitambulisho vya wachimbaji hao.

Uanzishwaji wa benki hiyo umelenga kutatua changamoto  ya ukosefu wa mitaji inayowakabili wachimbaji wadogo nchini jambo linalowasabisha washindwe kufanya uchimbaji wenye tija na kufikia malengo yao.

Akizungumza jijini hapa juzi wakati akisoma maazimio hayo, baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa Femata, Rais wa shirikisho hilo , John Bina alisema wadau  wa sekta ya madini wameishatoa michango yao ya awali ambapo hadi sasa zaidi ya Sh milioni 765 zimepatikana.

“Hii ni hatua  nzuri na niendelee kuwahakikishia wachimbaji  wadogo  wenzangu na watanzania kwamba  Femata imedhamilia kwa dhati kuhakikisha inakuwa na benki ya madini  na si ya Femata, benki hiyo itasimimiwa na Shirika la Madini la Taifa(STAMICO) pamoja na shirikisho,”alifafanua Bina.

Alisema ilikuhakikisha benki hiyo inaanza kutoa huduma mapema wameazimia kwamba Kamati ya Bunge ya Nishati na madini kuandaa kuandika andiko mradi la  kuchangisha pesa na chakula kitakachowakutanisha wabunge mbalimbali  kwa ajili ya kuchangia taasisi hiyo ya fedha itakayolenga kuwanufaisha wachimbaji wadogo.

 “Nitoe rai kwa  mabenki waendelee kuwakopesha wachimbaji wadogo  kwa  sababu na sisi tunaweza kuwa wadau muda si mrefu lakini niwaombe pia ndugu zangu wachimbaji wote kuhakikisha mnaiamini Femata lakini mnaitendea haki kwa kulipa ada ili  tuweze kujisaidia,” amesema Bina.

Bina alitaja maazimio mengine yaliyopitishwa kupitia majadiliano yaliyofanywa na wadau mbalimbali wa madini kwenye wiki ya madini kitaifa 2023 iliyofanyika jijini Mwanza kuanzai Mei 3 hadi 9, kongamano la wachimbaji wadogo wa madini na mkutano mkuu wa Femata ni Wizara ya madini  kukamilisha zoezi la kupitia tozo zinazotozwa na halmashauri kwa wachimbaji wadogo ili isiwe kikwazo  katika uchimbaji mdogo wa madini .

“Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kuendelea kufanya utafiti wa madini kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini na taarifa za tafiti ziwafikie wadau kwa wakati, mchakato wa utoaji  leseni kwa wachimbaji wadogo uwe wa wazi na unaozingatia sheria, kanuni na taratibu ili kuendana na haki kwa wachimbaji wadogo wanaoomba leseni kupitia Tume ya Madini,”alisema na kuongeza.

“Azimio lingine ni kuandaa mkutano mkuu wa  kitaifa utakaojadili changamoto na fursa zilizopo kwenye uchimbaji na biashara ya madini ya chumvi nchini itakayosimamiwa na Wizara ya Madini,”alieleza Bina.

Kwa mujibu wa Rais huyo lengo la Fematama ni kuchangia pato la taifa kwa asilimi 20 ifikapo 2028 na kuwaasa waandishi wa habari kutumia vizuri kalamu zao  kuandika  aina mbalimbali  ya madini yaliyopo Tanzania kwani itavutia wawekezaji katika sekta ya madini kutoka nje ya nchi hali itakayowezesha uanzishwaji wa soko la madini la Afrika hapa nchini kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Mgeni rasmi aliyefunga mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania, (TAWOMA) Taifa Semeni Malale, alisema ili Femata iweze kutimiza malengo iliyojiwekea  ni vyema wanachama wote wakashirikiana na kusameheana huku wakifanya shughuli zao kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles