23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Makala| Shule ya Sekondari High View yamuibua Atiki

Na Mwandishi Wetu

Imekuwa ni kawaida kwa Shule ya Sekondari ya High View na ya Msingi High Mount zilizopo Gongo la Mboto Mwisho wa Lami, Ilala jijini Dar es Salaam kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana.

Atiki Ally Atiki katikati akiwa na wanafunzi wenzake wakati akisoma shule ya sekondari High Vew, kushoto ni Faith Rwegasira na Kulia ni Kelvin Rwegasira.

Mkurugenzi wa Shule hiyo, Benard Kasika anasema miongoni wa vijana waliowaibua ni Atiki Ally Atiki (22) mzaliwa wa mkoani Mwanza ambaye kwa sasa yuko Marekani akiendeleza kipaji chake na Klabu ya Mpira wa Kikapu ya ya Brigham Youth Cougars ambako amesaini mkataba wa miaka minne na huku akiendelea na elimu ya juu ya Sekondari.

Mwaka 2018 walimpa ufadhili wa masomo ya Sekondari na Michezo katika shule ya Sekondari ya High View baada ya kubaini ana kipaji kikubwa cha mchezo wa mpira wa Kikapu wakiwa wamemtoa kwenye Kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete cha jijini Dar es Salaam.

Anasema Atiki alisoma hadi kidato cha pili kabla ya kupata ufadhili wa masomo na michezo nchini Canada mwaka 2020 katika kituo cha London Basket Ball Academy na sasa amehamia nchini Marekani ambako anasoma na huku akiendeleza kipaji chake  cha mchezo huo na kushiriki ligi ya vyuo vikuu ya mpira wa kikapu kwa nchi za Marekani na Canada.

Mkurugenzi huyo anasema kuwa ni matumaini yake kwamba Atiki atakuja kuwa mchezaji mkubwa wa mchezo huo siku za usoni.

“Ni imani yangu kuwa kijana huyu atakuwa nyota wa mchezo huo na atalitangaza jina la nchi yetu vema,” anasema.

Anafafanua kuwa mbali mbali na mchezo huo wa kikapu, pia shule yake ina endeleza vipaji vya michezo mbalimbali kama riadha,mpira wa miguu kwa watoto wa kike na wa kiume sanjari na michezo ya kuogelea.

“Nina waalimu wazuri sana wa michezo ambao ni Mwalimu, Rehema Mgunda na Mwalimu Fredrick Rwegasira,hawa ni walimu ambao pia wamemfundisha Atiki.

Mwalimu Mgunda na Rwegasira wanatoa wito kwa wazazi wenye watoto wenye vipaji wawapeleke shuleni hapo kwani ni ndiyo sehemu ambayo itatimiza ndoto za watoto wenye vipaji.

Imeandaliwa na Ino Communications 0754202450

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles