27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi Mwanga atoa vifaa vya michezo kwa shule za msingi

Safina Sarwatt, Mwanga

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Mwajuma Nasombe, ametoa vifaa mbalimbali vya michezo kwa shule za msingi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Umitashumta 2022.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo ofisini kwakwe Wilaya humo kwa Afisa Michezo, Denis Msemo amesema kuwa mwaka jana wilaya hiyo ilishika nafasi ya pili kwenye mashindano hayo kimkoa ambapo Manispaa ya Moshi ilishika nafasi ya kwanza.

Amesema kuwa Halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha inafanya Mapinduzi makubwa katika mashindano hayo kwani tayari wamekwisha fanya maandalizi mapema.

“Nina uhakika kwa Mwanga tumejipanga vema leo hii na kabidhi vifaa hivi vya michezo kama sehemu ya maandalizi yetu shule zote zinashiriki na tayari walimu wote wameshapewa maelekezo,” amesema Mwajuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles