24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kiruswa amtaka mmiliki wa mgodi wa Paramount Ltd kufuata taratibu

Na Mwandishi Wetu, Longido

NAIBU Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Longido mkoani Arusha, Dk. Steven Kiruswa ametoa agizo kwa mmiliki wa Mgodi wa PARAMOUNT LTD unaofanya shughuli za uchimbaji madini katika Kijiji cha Sinoniki na Kimwati katika Tarafa ya Engarenaibor wilayani Longido kuhakikisha anafuata taratibu za upataji wa ardhi kupitia kwenye mkutano mkuu wa Kijiji.

Dk. Kiruswa ametoa agizo hilo leo Alhamisi Januari 27, 2022 alipotembelea eneo la mgodi huo wilayani humo.

Ziara ikiendelea…

“Nimeona hapa Kimwati mmefuata utaratibu wote unaotakiwa, lakini Sinoniki hamjafuata taratibu naomba mkaliweke sawa hili kabla wizara haijachukua hatua kali za kisheria, lakini pia mkifuata taratibu mtaepuka migogoro na jamii,” alisema Dk. Kiruswa.

Aidha, Dk. Kiruswa amewataka kufuata taratibu zote za kisheria ili kuepuka migogoro na jamii ikiwemo masuala ya uhifadhi wa mazingira pamoja na kuweka makubaliano yenye kuonekana kwa jamii ikiwemo kusaidia miradi ya maendeleo.

“Nakuagiza Mwenyekiti wa Kijiji kaitisheni kikao cha Serikali ya kijiji hata cha dharura na kufikia wiki ijayo taarifa ya makubaliano hayo iwe imefika kwa Mkuu wa Wilaya Longido na sisi wizarani tutapata na kuangalia kama yapo sawa,” amesema Dk. Kiruswa.

Hata hivyo, amewashauri wawekezaji hao kufanya utafiti zaidi (Exploration) kabla ya kuanza uchimbaji au kuendelea kufanya uchimbaji kwa kukisia pasipo kuwa na uhakika pomoja na kuweka utaratibu wa kusoma taarifa za miradi waliyoitekeleza kwa jamii katika mikutano mikuu ya vijiji.

Katika hatua nyingine amewataka kutumia utaalamu wa kuchimba Madini aina ya vito ili kuepuka uharibifu wa mazingira kwani maeneo hayo ni maeneo ambayo hutumika kama korido ya wanyamapori na mifugo ya wananchi.

Dk. Kiruswa amewapongeza wawekezaji hao kwa kutoa fursa kwa vijana wazawa katika migodi hiyo,na kuwasisitiza kuwapa wanawake fursa za kuchakata mawe ili waweze kujiinua kiuchumi pamoja na kusisitiza ulinzi wa madini hayo pasipo kutorosha kupeleka nchi jirani kwani eneo migodi hiyo ipo mpakani na Meto nchini Kenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles