24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

MK Inc yamuibua upya A Flow Slim

KENTUCKY, MAREKANI

LEBO ya muziki yenye makazi yake Louisville, Kentucky nchini Marekani, MK Entertainment (MK Inc), imemuibua kivingine msanii wa kizazi kipya kutoka Burundi, Abdoul Kharim a.k.a A Flow Slim kupitia wimbo mpya, Come Closer.

Mk Visualiser ambaye ni Mkurugenzi wa lebo hiyo ameliambia MTANZANIA kuwa huo ni wimbo wa kwanza tangu A Flow Slim aingie mkataba na MK Inc hivyo anawaomba mashabiki wampokee na wampe sapoti kama wanavyowapa wasanii wengine.

“Video ya Come Closer tayari imetoka na inapatikana kwenye chaneli yake ya YouTube na mitandao mingine ya kusikiliza muziki. A Flow Slim ni msanii mwenye kipaji kikubwa hivyo kama sisi MK Inc tunavyompa sapoti basi na Afrika Mashariki yote pia imshike mkono,” alisema Visualiser.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles