‘On God’ ya Jesty B yaingia mtaani

0
390

WESTFALEN, UJERUMANI

MSANII wa kizazi kipya mwenye asili ya Nigeria anayeishi Westfalen, Ujerumani, Jesty B, amewaomba wapenzi wa muziki huo kuipokea video ya wimbo wake, On God, aliomshirikisha mwigizaji, Pitakwa.

Jesty ambaye ni mshindi wa tuzo kadhaa amewahi kujishindia tuzo kadhaa nchini Ujerumani, ameliambia MTANZANIA kuwa licha ya kufanya vizuri kwa jamii ya watu weusi Ulaya anatambua mchango wa mashabiki waliopo Afrika.

“Nimeshafanya makubwa hapa ‘Germany’, nimewahi kufanya kazi na mwigizaji nyota wa Nigeria, Victor AD, nimeshinda tuzo nyingi na sasa nataka kuwafikia mashabiki wa Afrika kwahiyo naomba sapoti katika video yangu, On God ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube,” alisema Jesty.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here