27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

MIUNDOMBINU INAKWAMISHA ELIMU NANYUMBU

Na ASHA BANI

HIVI majuzi nilikuwa wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara, kwa ajili ya kujionea hali halisi ya elimu na changamoto zake.

Nanyumbu katika matokeo ya elimu imeshika nafasi ya pili kutoka mwisho hasa katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka jana.

Hali hii hairidhishi hata kidogo hasa ukizingatia kwa sasa suala la elimu ni muhimu kwa kila mtoto.

Licha ya kwamba viongozi wa wilaya hiyo wamekuwa wakishughulikia changamoto zinazojitokeza ambazo ziko ndani ya uwezo wao, bado tatizo lipo kwa shule zilizopo nje ya uwezo wao.

Tatizo kubwa kwa wilaya hiyo ni kuwa na miundombinu isiyoridhisha kwa elimu ikiwa ni pamoja na umbali wa shule na maeneo wanayoishi wanafunzi. Miundombinu mibovu na ukosefu wa walimu ni jambo ambalo linahitaji usimamizi wa hali ya juu.

Ofisa Elimu Sekondari, Lwoga Musijaki anasema shule zilizopo wilayani humo hazina madarasa ya kutosha, ,nyumba za walimu na matundu ya vyoo.

Madarasa yanayohitajika kwa sasa ni 60 ambapo yaliyopo kwa sasa ni 84.

Nyumba za walimu zinazohitajika ni 324 zilizopo ni 43 hivyo pungufu ni 281; jambo ambalo linahitaji kufanyiwa michakato ya haraka ili kupatikana.

Mbali na hayo, kuna upungufu wa matundu ya vyoo, yaliyopo hayakidhi matakwa ya wanafunzi.

Licha ya changamoto za miundombinu, kuna haja ya kuhakikisha changamoto za  elimu kwa mtoto wa kike zinaangaliwa kwa ukaribu na kutatua matatizo yao.

Changamoto hizo ni pamoja na mimba za utotoni jambo ambalo linakatisha ndoto za wananfunzi hao.

Kwa mujibu wa Lwoga, tayari wanafunzi 23 wameachishwa shule kutokana na tatizo la mimba.

Katika hili, viongozi wa wilaya wanatakiwa kufanya kazi za ziada kuhakikisha wanatoa elimu kwa wanafunzi licha kwa kiasi fulani wameanza kufanikiwa.

Nasema kufanikiwa kutokana na watendaji wa Kata ya Nanyumbu wamekuwa wakitenga muda wao na kuzungumza na watoto wa kike kuwaelezea madhara ya kuanza kufanya ngono zembe wakiwa na umri mdogo jambo ambalo linakatisha ndoto zao.

Mkurugenzi wa halamashauri hiyo, Hamis Dambaya kwa kiasi kikubwa amekuwa akisisitiza kusimamia suala la elimu ili wilaya itoke katika nafasi ya aibu iliyopo sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles