27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mitandao yaua shamrashamra za Valentine

WAPENDAONA MWANDISHI WETU
IMEDAIWA kuwa kukua kwa sayansi na teknolojia na hasa matumizi ya mitandao ya kijamii, kumeua soko la kadi pamoja na maua yaliyozoeleka kununuliwa msimu huu wa Valentine.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wauza maduka ya kadi na maua katika maeneo mbalimbali ambao wanalalamikia kuporomoka kwa bidhaa hizo ambazo katika siku za nyuma zilikuwa zikiuzika kwa kiwango kikubwa.
Mmoja wa wauza duka hilo aliyejitambulisha kwa jina la Fadhili Muzo, alisema kwa mwaka huu hali ni mbaya zaidi kwani hakuna biashara ya kadi wala maua kama ilivyokuwa siku za nyuma.
“Mitandao ya kijamii imeua soko la kadi na maua kwani hata Kariakoo tunakonunua kwenye maduka ya jumla wanalalamikia suala hilo, watu wanatumia na kadi na maua kupitia What’sApp, Instagram, Facebookna Twitter,” alisema Muzo.
Mwingine Jenista Michael ambaye pia anauza duka, alisema kuna tofauti kati ya mwaka na mwaka katika kuadhimisha siku ya Valentine.
“Mimi nauza duka ambalo pia lina kadi na maua, nilitegemea msimu huu ndio biashara itachangamka na nitauza sana lakini imekuwa tofauti kwani wachache wananunua na ni wanafunzi lakini si kama miaka iliyopita,” alisema Jenista.
NayeRehema Suleiman ambayealikuwadukanihapoalishangaakuwa Valentine imewadianahukuakiwahajui.
“Hivi ni kesho (leo) aisee! Mimi sina habari kwasababu mara nyingi nimezoea kuona pilika za watu wakinunua kadi na wengine maua lakini huku sijaona. Mimi sijui kwanini imepoteza mvuto hii siku hata mwenyewe sikuhizi sina habari nayo,” alisema Rehema.
Gazeti hili lilizungumza na Mtaalamu wa Saikolojia na Uhusiano nchini, Dk. Chris Mauki ambaye alikuwa na maoni tofauti kwa kusema kwamba anachokiona kwa sasa ni mwamko wa watu katika masuala mazima ya uhusiano na ndoa.
“Hivi sasa shamrashamra ninazoziona tofauti na miaka mingine ni kwamba, mwaka huu watu wengi wanapenda kuboresha uhusiano wao, zamani walikuwa wanakunywa na kurudi lakini mwaka huu wanaboresha uhusiano kwa kukaa na kuzungumza na wenzi wao,” alisema Dk. Mauki.
Alisema jana alikuwa mkoani Arusha ambako waliandaa chakula cha jioni na kuzungumza na wapenzi na wanandoa kuhusu uhusiano na leo atakuwa Dar es Salaam kuendeleza kutoa somo la kuboresha uhusiano.
Gazeti hili lilifanikiwa kupita katika maeneo mbalimbali ya jiji kuanzia Posta Mpya mpaka Sinza na kuona baadhi ya maduka yakiwa yametundikwa nguo nyekundu lakini hakukuwa na shamrashamra za ununuzi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Kwa miaka mingi siku ya Valentine ilikuwa na umaarufu lakini utafiti mdogo uliofanywa na gazeti hili kwa mwaka huu, umegundua kuporomoka kwa umaarufu huo huku baadhi wakiwa hawaienzi tena kwa kununua zawadi kama maua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles