25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Misri yachunguza watalii kulishwa sumu

CAIRO, Misri

MAMLAKA nchini Misri zimeanzisha uchunguzi dhidi ya tukio la watalii kutoka Ulaya kuumwa ghafla baada ya kula chakula chenye sumu katika hoteli maarufu ya Red Sea mjini Hurghada.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu, watalii takribani 47, wakiwamo 29 kutoka Urusi na wanne wa Jamhuri ya Czech, walilazwa hospitali baada ya chakula hicho cha usiku.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imeweka wazi kuwa idadi kubwa ya watalii hao wamesharuhusiwa baada ya afya zao kuimarika lakini uchunguzi utafanyika kubaini kilichotokea.

Katika uchunguzi huo, tayari wafanyakazi watatu wa hoteli hiyo wameshawekwa chini ya ulinzi. “Mwanasheria Mkuu ameagiza kukamatwa kwa meneja wa chakula na vinywaji, meneja anayesimamia ubora, na mkuu wa kitengo cha mapishi,” imesomeka taarifa ya Mwendesha Mashitaka kupitia ukurasa wake wa Facebook.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles