30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuwaelimisha wananchi uelewa wa masuala ya fedha

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

KATIKA utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya sekta ya fedha wa mwaka 2020/2021-2029/2030 Serikali inakusudia kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo uelewa mdogo wa masuala ya fedha, bidhaa zitolewazo na watumiaji na watoa huduma za fedha na matumizi ya huduma za fedha zisizo rasmi huku ikiwaomba Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari kuwasaidia katika uelimishaji.

Hayo yameelezwa leo Novemba mosi mwaka 2022,na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba wakati akifungua kikao cha kuwajengea uwezo Wahariri wa vyombo vya habari kuhusu masuala ya fedha na maadhimisho ya wiki ya Huduma za fedha kitaifa.

Katibu Mkuu huyo amesema kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari kutambua umuhimu wa vyombo vya habari katika katika kuelimisha umma Wizara yake iliona ni vyema kuwapa mafunzo ili elimu watakayoipata waweze kuitumia kuelimisha jamii kuhusu masuala ya fedha.

Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwapa uelewa kuhusu mpango mkuu wa maendeleo ya sekta ya fedha,programu ya elimu ya fedha na maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha.

Katibu Mkuu huyo amesema kutokana na umuhimu wa sekta ya fedha katika kuchangia malengo ya Serikali ya kuleta maendeleo na kupinguza umaskini Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa mpango mkuu wa Maendeleo ya sekta ya fedha  wa mwaka 2020/2021-2029/2030.

Amesema mpango huo unatoa dira na mwelekeo wa sekta ya fedha kwa kipindi cha miaka 10 ambapo amedai masuala ya elimu ya fedha kwa umma  ni mojawapo ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa mpango huo.

Katibu Mkuu huyo amesema katika hatua za utekelezaji wa mpango huo Wizara imeandaa pia Programu ya kutoa elimu kwa umma ya mwaka ya mwaka 2021/2022-2025/2026 ambapo imeweka mikakati ikiwa ni pamoja na matukio na mbinu mbalimbali zitakazotumika katika utoaji wa elimu ya fedha kwa umma.

Amesema katika utekelezaji wa Mpango huo Serikali inakusudia kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo uelewa mdogo wa masuala ya fedha,uelewa mdogo wa bidhaa zitolewazo na watumiaji na watoa huduma za fedha na matumizi ya huduma za fedha zisizo rasmi huku ikiwaomba wahariri wa vyombo mbalimbali kuwasaidia katika uelimishaji.

“Katika kuhakikisha tunafikia malengo  Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa maadhimisho maadhimisho ya wiki ya Huduma za fedha ambapo kitaifa yatafanyika kuanzia Novemba 8-14 2021 katika viwanja vya Mnazi Mmoja  Jijini Dar es salaam,”amesema Tutuba.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Wahariri wa Wizara,Benn Mwang’onda amesema:

“Kama alivyosema Katibu Mkuu tuweze kuyakaribisha mafunzo haya na tusikilize yale ambayo wataalamu wetu wa Wizara ya Fedha ambayo wamedhamiria sisi tuyapate ili tuweze kufanikisha wiki ya huduma za kifedha”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles