NEW YORK, MAREKANI
VIFAA vinavyosadikiwa kuwa milipuko vimebainika katika nyumba ya Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton pamoja na Ofisi ya Barack Obama.
Taarifa hiyo imetolewa kwa vyombo vya habari jana na maafisa wa sheria.
Hiyo inakuja siku mbili tu baada ya bomu kurushwa katika nyumba ya mfadhili na mshauri wa mambo ya fedha, George Soros mjini hapa.
Clinton ni rais wa zamani wa Marekani na mkewe Hillary alijaribu kumrithi Obama urais mwaka 2016, akashindwa na Rais Donald Trump.
Taarifa zilizoripotiwa na New York Times zimesema vitu hivyo vilibainika kuwa vinalipuka baada ya fundi kuvifanyia uchunguzi.
Hata hivyo, msemaji wa Obama alikana kuwepo kwa tukio hilo na kuwataka waandishi kushirikiana na idara ya huduma ya maelezo ya siri.
Maofisa waandamizi wa Ikulu ya Marekani waliliambia Shirika la Habari la NBC kwamba Rais Trump tayari ameshapata taarifa kuhusu jambo hilo.