32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 1, 2023

Contact us: [email protected]

Trump aisuta Saudi Arabia kwa kuminya ukweli

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump amekiita kitendo cha Saudi Arabia kuminya ukweli juu ya mauaji ya mwandishi Jamal Khashoggi kuwa harakati mbaya zaidi katika historia.

Trump pia amesema yeyote aliyesuka mpango huo anatakiwa kuwa katika matatizo makubwa.

Marekani wamekuwa katika shinikizo la kuwabana washirika wao Saudi Arabia juu ya mkasa huo uliotokea katika ofisi za ubalozi mdogo nchi hiyo jijini, Istanbul, Uturuki.

Akiongea na wanahabari katika Ikulu ya White House, Trump alisema; “Walikuwa na wazo duni, na wakalitekeleza vibaya mno, na kiufupi harakati zao za kuuminya ukweli ndio mbovu zaidi katika historia ya kujaribu kuficha ukweli.

“Naamini aliyekuja na wazo lile yupo katika matatizo makubwa hivi sasa. Na wanatakiwa kuwa kwenye matatizo.”

Punde tu baada ya kauli ya Trump, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo alitangaza kufutwa hati za kusafiri za kuingia Marekani kwa watu 21 wanaoshukiwa kutekeleza mauaji hayo.

Mamlaka za Saudi Arabia zimekuwa zikitoa taarifa za kujikanganya juu ya tukio hilo la kuuwa kwa mwandishi huyo ambaye alikuwa kinara wa kumkosoa Mrithi wa Kiti cha Ufalme, Prince Mohammad bin Salman.

Khashoggi aliingia katika ofisi hizo za ubalozi mdogo Oktoba 2, mwaka huu kushughulikia nyaraka za ndoa na hakutoka tena.

Awali Saudi Arabia walisema alitoka hai, lakini baada ya shinikizo kubwa kutoka Uturuki na jumuiya ya kimataifa, ikakiri kuwa aliuawa wakati alipojaribu kupambana.

Lakini juzi na jana Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan alisisitiza kuwa mauaji ya Khashoggi yalipangwa siku kadhaa kabla ya kutekelezwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles