25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 220/- kumrejesha Okwi Simba

 Emmanuel Okwi
Emmanuel Okwi

 

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Simba umepanga kutoa kitita cha Dola 100,000 za Marekani (sawa na Sh milioni 220 za Kitanzania) ili kumrejesha kikosini mshambuliaji wao wa zamani, Emmanuel Okwi.

Kwa sasa Okwi anakipiga katika klabu ya SønderjyskE inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Denmark ‘Superliga’, ambayo alisaini mkataba wa kuichezea hadi Juni 30, mwaka 2020.

Straika huyo raia wa Uganda, amefanikiwa kuifungia timu yake ya SønderjyskE bao moja katika ligi kuu msimu huu na jingine kwenye michezo ya kufuzu kucheza Ligi ya Ulaya.

Okwi aliyecheza Simba kwa mafanikio makubwa tangu msimu wa 2010 /11,  hakufanikiwa kufunga bao lolote msimu wa 2015/16  alipojiunga na timu ya SønderjyskE.

Kwa mujibu wa mtandao wa soka25east wa nchini Uganda, imedaiwa kuwa viongozi wa Simba tayari wamefikia makubaliano na kutakiwa kuilipa klabu ya SonderjyskE kiasi cha Sh milioni 220.

Imeelezwa kuwa Okwi yupo tayari kurejea na kukipiga katika kikosi cha Simba na kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inaongozwa na Laudit Mavugo, Shiza Kichuya na Ibrahim Ajib.

Simba inaongoza ligi kwa kufikisha pointi 35 baada ya kushuka dimbani mara 15 na kushinda michezo 11, kupata sare mbili na kufungwa mechi mbili.

Gazeti hili lilipomtafuta Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele, kuzungumzia suala hilo, hakutaka kuweka wazi licha ya kudai ni kweli  baadhi ya wadau wanalizungumzia na kulipigia chapuo.

‘Klabu ina wadau, hivyo mdau yeyote anaweza kujisikia na kuibuka kama wewe akafanya mambo yake kufika kwenye timu ukamkuta mchezaji,” alisema Kahemele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles