24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Beyonce, Jay Z waangukia kwa Michelle Obama

beyonce-jay-z

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya Hillary Clinton kushindwa katika uchaguzi mkuu nchini Marekani dhidi ya Donald Trump, nyota wa muziki nchini humo, Jay Z na mke wake, Beyonce, wamemtaka mke wa Barack Obama, Michelle Obama, awanie kiti hicho 2020.

Wasanii hao walikuwa wanamsapoti Hillary katika uchaguzi huo na walikuwa wanaungana baadhi ya sehemu kwa ajili kumnadi, lakini hajafanikiwa kushinda, hivyo wawili hao wameamua kuangukia kwa mke wa Obama, Michelle, kuwa awanie nafasi hiyo mwaka 2020 wataungana pamoja kwenye kampeni.

Michelle na mume wake, Obama, ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanampigia debe Hillary, lakini hawakufanikiwa.

Novemba 7 mwaka huu, Jay Z aliachia wimbo mpya ambapo ndani yake kuna mistari inasema kuwa anataka mtoto wake akue huku akiwa anaongozwa na rais mwanamke na hivyo walitamani kuona Hillary kupata nafasi hiyo.

“Nilitamani kuona mtoto wangu akiwa anakua chini ya rais mwanamke, Hillary hajapata nafasi hiyo, lakini ninaamini bado kuna nafasi nyingine baada ya miaka minne ijayo, nimekuwa nikiongea na Michelle mara kwa mara na ninaamini atafanya hivyo,” alisema Jay Z.

Wasanii mbalimbali wameonesha kuguswa na uchaguzi huo, huku wengine wakionesha kuwa tofauti na matokeo hayo.

Lady Gaga

Nyota huyo wa muziki nchini Marekani, juzi alionekana mtaani akiwa amevaa T-shirt ambayo inaonesha kumpenda Rais Mteule, Donald Trump.

Msanii huyo alionekana katika mitaa ya jiji la New York akiwa amevaa T-Shirt nyeupe yenye maandishi mekundu ambayo yanasema ‘Nakupenda Trump’.

T.I

Rapa T.I kwa upande wake amempa pole rais ambaye anamaliza muda wake, Barack Obama, kwa mteja wake kushindwa katika uchaguzi huo.

“Pole kwa matokeo ambayo kuna baadhi ya watu hawakuyatarajia, lakini tunafurahi tulikuwa na wewe kwa kipindi chote, lakini sasa tunasubiri kinachofuata,” alisema T.I.

Snoop Dogg

Rapa huyo ameonekana kumshambulia Hillary kwa kushindwa uchaguzi huo. Snoop amedai kuwa Hillary ameshindwa mbele ya mtu dhaifu.

Hata hivyo, rapa huyo alionekana kutumia maneno makali kwa Hillary na pia amedai kuwa Obama hakuwa na timu mzuri ya kuweza kuwashawishi watu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles