23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Milio ya risasi yazua taharuki Mbande

bastolaNA TUNU NASSOR,-DAR ES SALAAM

TAHARUKI imetokea juzi usiku katika eneo la Mbande wilayani Temeke, baada ya kuwapo kwa milio ya risasi mfululizo kwa zaidi ya saa moja.

Wakazi wa eneo hilo walidai kuwa tukio hilo lilianza kutokea saa nne usiku wa kuamkia jana.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Abdallah Issa, alisema milio hiyo haikuwa ya kawaida hali iliyowapa hofu.

“Ilikuwa saa nne usiku ambapo tulisikia milio ya risasi mfululizo tukajiuliza kinachoendelea, kwa kuwa tumewahi kukumbwa na matukio kama haya tukadhani tumevamiwa na majambazi,” alisema Issa.

Kutokana na hali hiyo, alisema walijikuta wanajawa na hofu na kukimbia kutafuta mahali pa kujificha bila kujua kinachoendelea hadi hali ilipotulia.

Naye Mwajuma Kombo, alisema alihaha kutafuta pa kuwaficha watoto wake kwa kuwa aliamini kuwa walivamiwa na majambazi katika mtaa wao.

“Jana (juzi) usiku ilikuwa tafrani baada ya kusikia milio hiyo nilikimbia na kutafuta pa kuwaficha wanangu wawili ambao bado ni wadogo sana nikiamini tayari tumevamiwa na majambazi tena,” alisema Mwajuma.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto, alisema wananchi waondoe hofu kwa kuwa milio hiyo ilitokana na mafunzo ya upigaji risasi kwa mgambo.

“Ni kweli imetokea lakini milio hiyo ilitokana na wanamgambo waliokuwa wakijifunza kulenga shabaha katika eneo hilo,” alisema Muroto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles