Florence Sanawa, Tandahimba
Halmashauri ya wilaya Tandahimba imetenga zaidi ya Sh milioni 47.4 kwa ajili ya ukarabati wa wodi ya wanaume na kliniki ya meno.
Katibu wa Afya wa halmashuri hiyo, Faustine Pamba amesema hayo jana wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Yusuph Nannila na kamati ya siasa ya mkoa ya chama hicho kukagua miradi ya maendeleo wilayani Tandahimba.
Amesema ukarabati huo wa miundombinu umefanywa baada ya kuona upungufu hasa kwa wodi ya wagonjwa wanaume kliniki ya meno.
“Ili kukamilisha ukarabati wa miundombinu, magari na vifaa tiba pia ilitenga Sh milioni 70 kutoka katika vyanzo hivyo.
“Ukarabati huu ulifanywa ili kupunguza changamoto ya wodi ya wanaume ambayo haikuwa na stara huku chumba cha meno kikiwa hakina usiri hali iliyokuwa haileti picha nzuri kwa wagonjwa wanaofuata matibabu katika hospitali hiyo,” amesema.