SADC yataka Zimbabwe iondolewe vikwazo

0
1395
Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Rais Zimbabwe (walioshikana mikono) wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), uliomalizika jijini Dar es Salaam leo. PICHA NA SILVAN kIWALE

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wamekubaliana kuendelea kuiunga mkono nchi ya Zimbabwe iondolewe vikwazo ilivyowekewa ili nchi hiyo iweze kukua kiuchumi.

Rais na Mwenyekiti wa Mkutano huo, Dk. John Magufuli, amesema hayo leo Jumapili Agosti 18, katika siku ya pili na ya mwisho ya mkutano huo ulioanza jana jijini Dar es Salaam.

“Kuhusu Zimbabwe tumekubaliana kuwa tuendelee kufanya mawasiliano na jumuiya za kimataifa ili kuwezesha kuondolewa kwa vikwazo kwenye nchi hiyo ikiwamo kupitia mabalozi zetu pamoja na jumuiya mbalimbali.

“SADC kwa pamoja viongozi wote kwa kauli moja tunatamka tuko pamoja na Zimbabwe na hatutaiacha,” amesema Rais Dk. Magufuli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here