29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mifuko ya plastiki pasua kichwa

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

MIEZI kadhaa baada ya Serikali kufanikiwa kupiga marufuku mifuko ya plastiki, kumeibuka matumizi ya vifungashio vya plastiki vya bidhaa kama mbadala jambo linalowapa wakati mgumu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Itakumbukwa Juni Mosi mwaka jana ilikuwa ni mwisho kutumika kwa mifuko ya plastiki kwa sababu ilikuwa ikichochea kwa asilimia kubwa kuchafua mazingira.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau wa mifuko mbadala Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Zungu, alisema pamoja na kudhibitiwa kwa mifuko ya plastiki, lakini bado matumizi yake yanaendelea kupitia vifungashio.

Zungu alisema kumeibuka tabia ya matumizi ya vifungashio vya plastiki kutumika kama mifuko kinyume na sheria, ambapo wachuuzi wamekuwa wakiitumia kuwekea bidhaa tofauti na ilivyokuwa imekusudiwa.

“Nilikwenda Soko la Kisutu nikauziwa bidhaa na kupewa kifungashio cha plastiki kwa madai kuwa ndiyo mifuko inayoruhusiwa jambo ambalo linaongeza matumizi ya mifuko hiyo.

“Sheria inaelekeza kwamba mtengenezaji wa vifungashio hivyo anatakiwa kuvipeleka moja kwa moja kwa mteja wake ambaye ndiye anayehifadhia bidhaa na si mtengenezaji kupeleka vifungashio hivyo sokoni. 

“Hivyo kuanzia sasa anayetengeneza vifungashio anatakiwa kuweka jina na anuani yake katika vifungashio hivyo ili vikitumika vinginevyo tuweze kumpata,” alisema Zungu.

Aidha, katika hatua nyingine aliwataka wadau hao kufikiri na kuja na njia mbadala kwa wafua nguo ‘dry cleaners’, na wapishi wa mikate ambao wamekuwa wakitumia mifuko ya plastiki kuhifadhia.

“Bado kuna changamoto kwa hawa watu wanaofanya kazi ya kufua nguo pamoja na wale wapishi wa mikate ambao wamekuwa wakitumia mifuko hii kuhifadhia, jambo ambalo ni changamoto.

“Hivyo lazima sasa wadau muangalie namna ambavyo mtaweza kutumia mifuko ya karatasi katika uhifadhi wa nguo na mikate,” alisema Zungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles