Na Sheila Katikula, Mwanza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amezitaka bodi kusimamia matumizi ya yasiwe makubwa kwenye mifuko ya sekta ya shirikisho la mashirika ya hifadhi ya Jamii nchini ili yasizidi matumizi  na kupelekea kushindwa kufikia malengo ya kutoa mafao kwa wanachama.
Waziri huyo, ametoa wito huo leo Desemba 22, jijini Mwanza wakati wa kufunga mkutano wa jumbe wa shirikisho la mashirika ya hifadhi ya Jamiii nchi (TSSA) amesema bodi inajukumu la kushauri na kusimamia uwekezaji unaofanywa na  mifuko ya hiyo  kwa lengo la kulinda fedha za wanachama.
Amesema mifuko ya hifadhi ya jamii inajukumu la kushauri na kuona kwenye viwanda vinyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi hapa nchi na siyo kuagiza nche ya nchi kwani ni vema kuanzisha vya hapa nchini amvavyo vitakavyotoa ajira na kuongeza idadi ya wanachama vitakavyosaidia kupanua wigo wa sekta hiyo.
“Inasikitisha kuona hata dripu la maji ya kumwekea mgonjwa tunashindwa kuzalisha tunaagiza kutoka nje wakati uwezo wa kuanzisha viwanda tunao nitafarijika zaidi nitakapo sikia kuwa malengo haya yametimizwa na viwanda hivyo vinatoa ajira kwa vijan,” amesema Mhagama.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto, Prof. Mabula Mchembe ameishukuru TSSA kwa kutoa mafunzo hayo ya siku tatu yenye lengo la kutambua jinsi ya uendeshaji wa mfuko ya hifadhi ya jamii katika uwekezaji wa viwanda.
Aidha, Mwenyekiti wa TSSA, William Erio amesema watafanya mpango wa kufufua kiwanda cha nyama cha Busisi ili kiweze kufanya kazi na vijana waweze kupata ajira.