22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Michuano ya Uefa kuendelea leo

Germany Soccer Champions League FinalLONDON, ENGLAND

MICHEZO ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inatarajia kuendelea leo katika viwanja mbalimbali, ambapo michezo nane itapigwa.

Katika kundi E, Barcelona watakuwa kwenye Uwanja wa nyumbani Camp Nou na kuwakaribisha wapinzani wao, Bayern Leverkusen, kutoka nchini Ujerumani, mchezo ambao unaonekana kuwa na mvuto wa aina yake.

Katika mchezo wa kwanza wa michuano hii Barcelona ilikutana na AS Roma na matokeo yakawa 1-1, hata hivyo, katika mchezo wa leo Barcelona itakuwa na wakati mgumu kwa kuwa itamkosa mshambuliaji wake, Lionel Messi, ambaye aliumia goti mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo atakaa nje ya uwanja kwa wiki saba hadi nane.

Katika Uwanja wa Borisov Arena, Bate watakuwa nyumbani na itawakaribisha As Roma, katika mchezo wa awali Bate ilikubali kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Bayer Leverkusen.

Katika kundi F, Arsenal ya nchini England itapambana na Olympiakos ya nchini Ugiriki, wakati mchezo wa awali Arsenal ilikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Dinamo Zagreb, wakati Olympakos ikipokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Bayern Munich.

 

Miamba kutoka nchini Ujerumani, Bayern Munich, watashuka dimbani kupambana na Dinamo Zagreb kutoka nchini Croatia.

 

Michezo mingine ambayo itapigwa leo ni pamoja na FC Porto ambayo itapambana na Chelsea katika kundi G, huku Maccabi Tel Aviv ikipambana na Dynamo Kiev, wakati kundi H, Lyon ikicheza dhidi ya Valencia, huku Zenit St Petersburg ikipigana na KAA Gent.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles