27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Michoro Sports Arena yamkosha Sanga

NA MWANDISHI WETU

BAADA ya Serikali kukamilisha michoro ya ujenzi wa ukumbi mkubwa kwa ajili ya michezo na Sanaa za ndani ‘Sports and Arts Arena’, Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga, amesema lilikuwa ni ombi lake kwa Serikali wakati wa kuchangia Bajeti ya Wizara ya Mwaka 2021/2022.

Kwa mujibu wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, Serikali imekamilisha michoro ya Ukumbi mkubwa kwa wa michezo na Sanaa za Ndani (Sports and Arts Arena) utakaokuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 15,000 ambao kujengwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma.

Sanga amesema alisimama na kuomba Serikali kuanza mchakato wa ujenzi wa Sports Arena na jana Serikali imeonyesha michoro ya Arena hizo ikiwa ni hatua ya kuinua michezo nchini.

Wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Michezo ya 2021/2022 Bungeni, Sanga alisema “Tunaomba Arena zijengwe, ngumi na michezo mingine inakuwa nchini tunahitaji kumbi za kufanyia matukio hayo, Taifa bila Arena tunakuwa bado tupo zama za ukoloni”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles