30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mwaka mmoja wa Rais Samia, Mchengerwa aanika mafanikio michezoni

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali imekamilisha hatua muhimu za ujenzi wa miundombinu muhimu ya michezo ikiwemo kukamilika kwa usanifu wa Uwanja wa Soka Dodoma, kukamilika usanifu wa ujenzi wa viwanja vya mazoezi na kupumzikia wananchi vitakavyojengwa Dar es Salaam, Dodoma na Geita.

Pia kukamilika kwa michoro ya ukumbi kubwa kwa ajili ya michezo na Sanaa za ndani (Sports and Arts Arena) utakaokuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 15,000 na kujengwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma.

Mchengerwa ameyasema haya kwenye Mkutano na waandishi wa Habari leo Machi 16, 2022 wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Wizara yake kwa kipindi hiki ambapo amesisitiza kuwa hatua za kuanza ujenzi wa miradi hii zinaendelea vizuri

Aidha, amesema jambo jingine la kimkakati sana na litakalosaidia kulea vipaji mbalimbali vya michezo ni uamuzi wa Serikali kuridhia kuanzisha shule maalum 56 (sports academies) zitakazokuwa kila mkoa nchini ambapo amefafanua kuwa jumla ya shilingi bilioni 19 zitatumika kukarabati shule hizo na kuwekewa miundombinu mbalimbali ya kisasa.

“Hili nalo ni jambo la kihistoria linalokwenda kuzalisha vijana walioiva tangu wadogo iliwaiwakilishe nchi yetu ndani nje ya nchi kwa ufanisi,” ameeleza.

Pia amefafanua kuwa Novemba mwaka jana Tanzania ilipata bahati ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Soka kwa Walemavu Afrika (CANAF-2021) ambapo pamoja na Tanzania kuzipokea takribani nchi 13 kutoka Afrika.

Amesema Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Walemavu, Tembo Warriors, ilikuwa miongoni mwa Timu nne zilizofuzu kutoka Afrika kwenda Kombe la Dunia Uturuki Oktoba mwaka huu.

“Mhe. Rais aliagiza maandalizi ya timu hii yaanze, naomba leo kutoa taarifa kuwa tayari timu hii imeshaingia kambini jijini Dar es Salaam tangu Februari 20 mwaka huu ikiwa chini ya ufadhili wa Serikali moja kwa moja”. Ameongeza Mhe, Mchengerwa.

Pia amesema katika kipindi hiki na hasa baada ya hotuba ya Rais Bungeni iliyokuwa na maelekezo mahsusi, Wizara imeweka kipaumbele maalum katika kuongeza hamasa kwenye michezo kwa wanawake ikishirikiana na mashirikisho na vyama mbalimbali.

Amesema moja ya mafanikio makubwa ni Wizara kukutana mwaka jana na wadau wengi wa michezo kwa wanawake na matokeo yake ni kuanzishwa kwa Tamasha la Kwanza nchini la Michezo kwa Wanawake la Tanzanite lililofanyika Septemba 16 -18, 2021, Dar es Salaam na kushirikisha wanawake zaidi ya 350 ambao walionyesha vipaji vyao katika michezo ya jadi (kuruka kamba, rede, ngoma na kukuna nazi), riadha, soka, mpira wavu, mpira wa kikapu, karate na kutunisha misuli.

Aidha, amesema Serikali iliongeza bajeti ya kuhudumia timu za Taifa kwa ujumla kutoka Shilingi milioni 320 hadi zaidi ya bilioni 1.3, fedha ambazo hizi zinaweza kuwa ndogo lakini zimeleta ari kubwa na mojawapo ni mafanikio ya Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, ambayo imeendelea kutwaa vikombe vya Cosafa kwa miaka mitatu mfululizo.

Amewahamasisha watoto wa kike kote nchini kushiriki kwa wingi katika michezo, fursa zaidi kwa sasa zinaendelea kufunguka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles