32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mhagama ataka nguvu itumike kukabili njaa

JenistaNa Mwandishi Maalumu, Dodoma

WAZIRI wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, kuhakikisha anatumia nguvu katika kuwalazimisha wananchi kulima ili kukabiliana na tatizo la njaa ambalo limekuwa likiukabili Mkoa wa Dodoma.

Mhagama aliyasema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wakulima wa zao la mhogo ambao walihamasishwa kulima zao hilo linalostahimili ukame ili kukabiliana na njaa.

Alisema katika kuhakikisha tatizo la njaa linakwisha mkuu wa wilaya huyo anatakiwa kuweka mikakati mipya ambayo itakuwa na tija katika kuhakikisha njaa inakwisha wilayani hapo.

“Kama mtaendelea na mikakati yenu ya kila siku tatizo la njaa halitakwisha mnatakiwa hivi sasa kutumia nguvu lazimisheni wananchi walime mazao yanayostahimili ukame kama mihogo na mtama,” alisema Mhagama.

Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kitengo cha maafa ilitoa Sh milioni 35 kwa ajili ya kununua mbegu za mihogo na mtama kwa wananchi ya wilaya hiyo waliokuwa wanakabiliwa na baa la njaa.

Aliongeza kuwa kwa namna alivyojionea maendeleo ya baadhi ya wakulima waliolima mihogo wameweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na baa la njaa kwa kipindi kirefu.

“Kwa hali hii basi sisi kama ofisi ya waziri mkuu hatuna haja ya kuendelea kuleta chakula cha msaada tena huku kwakuwa zao la mihogo ambalo sisi tulileta mbegu imeweza kuwasaidia wakulima kuondokana na njaa lakini pia wengine wamejenga nyumba na kuezeka kwa bati,” alisema Mhagama.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Utaly, alisema kuwa watapanga kuhamasisha kilimo cha zao hilo la muhogo ambalo limeonekana kuwa mkombozi wa njaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles