27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Afrika yajikongoja ukuaji wa uchumi

Na Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

UKUAJI wa Pato la Ndani (GDP) katika nchi za bara la Afrika umekabiliwa na changamoto ya uzalishaji duni.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya uchumi ya Shirika la Wahasabu Wasajiliwa wa England na Wales (ICAEW), ilieleza kuwa hatua hiyo inatokana na kushuhudiwa kwa nchi ya Kenya ambayo inakabiliwa na uzalishaji wa kiwango cha chini hasa katika sekta ya kilimo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa katika kipindi cha miaka 15 iliyopita biashara na uwekezaji ilikuwa ikilinda bara hili dhidi ya mgogoro wa kifedha duniani.

Chombo hicho cha uhasibu na fedha, kimefichua uzalishaji wa kiwango cha chini pamoja na uwapo wa fursa kubwa ya kiuchumi.

“Ripoti inagusia kuwa kuanzia mwaka 2000 hadi 2015, wastani wa ukuaji wa GDP barani Afrika ulikuwa asilimia 4.8 kwa mwaka, ukiwa ni zaidi ya asilimia 2.3 kamili ya kiwango cha wastani wa dunia wakati wa miaka ya 1990. Hata hivyo, kiwango hicho kwa namna fulani ni cha chini kulinganisha na ukanda wa ASEAN (Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia), ambao ulikuwa kwa asilimia 5.6 kwa mwaka na asilimia 0.2 zaidi ya wastani wa ukanda wa Mashariki ya Kati,” ilieleza ripoti hiyo.

Mkurugenzi wa ICAEW Kanda ya Mashariki ya Kati, Afrika na Asia Kusini, Michael Armstrong, alisema: “Ulinganifu wa ufanisi wa baadhi ya masoko ya kanda nyingine zinazokuja juu kiuchumi linapokuja suala la thamani unaonekana kutia moyo. Lakini ukweli ni kuwa Afrika inaanza na kiwango cha chini cha maendeleo ya uchumi kuliko chumi hizo nyinginezo.

“Nchi za Afrika zinapaswa kuboresha uzalishaji katika sekta ya kilimo, kutokana na uwapo wa gharama ndogo za nguvu kazi na hali ya hewa ifaayo. Hata hivyo, maendeleo yanaonesha kukatisha tamaa. Ripoti inaonesha kuwa ukanda wa Afrika Mashariki umekumbwa na mfumuko wa bei,” alisema.

Alisema mvua zilizonyesha hivi karibuni zimesababisha kupaa kwa bei ya vyakula katika nusu ya eneo la Kusini mwa Afrika, huku kukiwa na mvua ya kiwango cha juu kuliko kawaida nchini Tanzania na Kenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles