Ramadhan Hassan,Dodoma
Naibu Waziri wa Kilimo,Omari Mgumba amesema Serikali inakamilisha kuunda upya Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania.
Kauli hiyo ameitoa Leo bungeni Mei 24 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,Sikudhani Chikambo(CCM).
Katika swali lake,Chikambo ametaka kujua lini Serikali itachukua hatua ya kuunda tena Bodi ya Korosho na kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kama ilivyo mazao mengine.
Akijibu,Mgumba amesema Serikali inakamilisha kuunda upya Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania.
“Uteuzi utatangazwa na Mamlaka ya uteuzi muda mfupi ujao kwa mujibu wa katiba sheria na kanuni zilizopo,” amesema Mgumba.