Mnyika ahoji tatizo la umeme jimboni kwake

0
2859

Ramadhan Hassan ,Dodoma

Mbunge wa Kibamba,John Mnyika amehoji ni kwanini tatizo la kukatika kwa umeme katika Jimbo lake.

Akiuliza kwa niaba Mnyika,Mbunge wa Ubongo,Saed Kubenea Leo bungeni Mei 24,amehoji kuhusiana na tatizo la kukatika umeme katika Jimbo la Kibamba.

“Je, ni kwanini tatizo la kukatika umeme katika Jimbo la Kibamba halijapatiwa ufumbuzi.

” Je,maeneo gani mpaka sasa Tanesco haijafikisha umeme,”amehoji.

Akijibu,Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu amesema kukatika kwa umeme inatokana na zoezi la kuhamisha miundombinu ya umeme ili kupisha upanuzi wa barabara ya Dar es salaam -Morogoro.

Amesema maeneo ambayo hajapatiwa umeme katika Jimbo hilo ni,Kibesa,Kisopwa,Kipera,Msumi na baadhi ya maeneo ya Mpigi na Kwembe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here