Na ANNA RUHASHA, MWANZA
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Sengerema kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Hamisi Tabasamu amehaidi kuwa iwapo atachaguliwa na wananchi kuwa mbunge wa jimbo hilo, atajenga kituo cha kulelea wazee.
Ahadi hiyo aliitoa wakati akizungumza na baadhi ya wazee walika walioshiriki katika kikao ndani kilichofanyika katika ukumbi wa Mayengela mjini Sengerema mkoani Mwanza.
Alisema kwa kutambua mchango wa wazee ambao wengi wao hawapati nafasi ya kushiriki mikutano ya kampeni zinazoendelea, aliona aitishe kikao ili awaeleze mambo atakayofanyia akichaguliwa.
“ Wazee wangu nimewaomba tukutane katika kikao hiki ili niwaeleze vipaumbele vyangu, kipaumbele changu kwenu nikuwajengea kituo cha kisasa, najua mnajua tulivyokuwa tukishirikiana na nyinyi kwa kipindi chote kabla sijawa na ndoto za kugombea ubunge,’’alisema Tabasamu.
Alisema baadhi ya wazee wamekuwa wakihangaika mitaani bila kujua hatima ya maisha yao ambapo alisema kwa mara ya kwanza wataonja ladha ya kuwa na mbunge ambaye anatakuja kuwaunganisha pamoja na kupunguza changamoto walizonazo .
“ Natambua kuna wazee wastaafu, kunabaadhi ya wazee humu mmefukuzwa na watoto wenu, kuna wazee mmefiwa na waume zenu, wake zanu na baadhi watoto wenu ambao mlikuwa mkiwategemea wametangulia mbele za haki, mimi Tabasamu nikichaguliwa lazima niwanjengee kituo ili iwe raisi kupata huduma haraka mnazostahili,’’alisema Tabasamu.
Tabasamu alisema kutokana na changamoto hizo atajenga kituo ambacho kitatoa huduma zote muhimu zikiwemo, za matibabu, viwanja vya kufanyia mazoezi, gari la na kuweka wataalamu mbalimbali watakao wahudumia wazee hao.
“Wazee wangu natambua Serikali inavyowajali kuna wazee hapa wanakadi za matibabu bila malipo, nitumie nafasi kuwaomba kura kwa chama cha mapinduzi ambacho kinaleta maendeleo kwenu pia katika uongozi wangu nitatenga muda wa baada ya miezi mitatu kuzungumza na nyinyi,” alisema Tabasamu.