26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Mgombea ubunge aahidi kujengea wazee kituo cha kisasa

Na ANNA RUHASHA, MWANZA

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Sengerema kupitia tiketi ya Chama  Cha Mapinduzi  (CCM ) Hamisi Tabasamu amehaidi kuwa iwapo atachaguliwa na wananchi kuwa mbunge wa jimbo hilo, atajenga kituo cha kulelea   wazee.

Ahadi hiyo aliitoa wakati akizungumza  na  baadhi  ya wazee  walika walioshiriki katika kikao ndani  kilichofanyika katika ukumbi wa Mayengela mjini Sengerema mkoani Mwanza.

 Alisema kwa kutambua mchango wa wazee  ambao  wengi wao hawapati nafasi ya kushiriki mikutano ya kampeni zinazoendelea, aliona aitishe kikao ili awaeleze  mambo atakayofanyia  akichaguliwa.

“ Wazee  wangu nimewaomba  tukutane katika kikao hiki ili niwaeleze vipaumbele  vyangu, kipaumbele  changu  kwenu nikuwajengea  kituo cha kisasa, najua  mnajua    tulivyokuwa tukishirikiana na nyinyi kwa kipindi chote  kabla sijawa na ndoto za kugombea ubunge,’’alisema  Tabasamu.

 Alisema baadhi  ya  wazee  wamekuwa  wakihangaika mitaani bila kujua  hatima ya maisha yao ambapo  alisema kwa mara ya kwanza wataonja ladha ya kuwa na mbunge  ambaye  anatakuja kuwaunganisha pamoja   na  kupunguza  changamoto  walizonazo .

“ Natambua  kuna  wazee  wastaafu, kunabaadhi ya wazee  humu mmefukuzwa na watoto wenu, kuna wazee mmefiwa na waume zenu,  wake zanu na baadhi watoto wenu ambao mlikuwa mkiwategemea  wametangulia  mbele za haki, mimi Tabasamu  nikichaguliwa  lazima  niwanjengee kituo ili iwe  raisi kupata  huduma  haraka mnazostahili,’’alisema  Tabasamu.

 Tabasamu  alisema kutokana  na changamoto  hizo     atajenga kituo ambacho kitatoa huduma zote muhimu    zikiwemo, za  matibabu, viwanja vya kufanyia mazoezi,   gari la na  kuweka  wataalamu mbalimbali  watakao wahudumia wazee hao.

“Wazee wangu  natambua  Serikali  inavyowajali kuna  wazee  hapa  wanakadi  za matibabu  bila  malipo, nitumie  nafasi kuwaomba  kura kwa  chama cha  mapinduzi  ambacho  kinaleta  maendeleo  kwenu  pia  katika  uongozi  wangu  nitatenga   muda wa  baada ya miezi mitatu  kuzungumza na  nyinyi,” alisema  Tabasamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles