25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa tuhuma za kuua akijaribu kutoa mimba

Na Nyemo Malecela, Kagera

JESHI la Polisi mkoani Kagera linamshikiria Frodius Protace ‘Gafseki’ (24) mkazi wa Kijiji cha Rushe wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua Saraiya Idd (25) mkazi wa Kijiji cha Mabuye wilayani Misenyi wakati akijaribu kumtoa mimba ya miezi sita kwa malipo ya Sh 600,000.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi alisema mwili wa marehemu uligundulika Oktoba 12 mwaka huu ukiwa umezikwa katika shamba la Anastela Jacob (47).

“Baada ya mwili huo kufukuliwa chini ya usimamizi wa Polisi, tukio hilo liliripotiwa kama kifo chenye mashaka kwa sababu ya kutotambulika lakini pia kukutwa na dalili za kutolewa mimba na kutokwa damu nyingi sehemu za siri na kuwekwa pamba puani.

“Kufuatia uchunguzi uliofanywa, polisi ilifanikiwa kupata taarifa za mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo ndipo alikamatwa na kufanyiwa upekuzi katika makazi yake,” alisema.

Malimi alisema baada ya kufanyiwa upekuzi katika chumba alichokuwa akiishi kulipatikana matandiko kitandani yenye damu na kitambulisho cha mpiga kura cha marehemu.

Aidha Malimi alisema katika mahojiano mtuhumiwa alikiri kushiriki mafunzo ya kozi fupi ya ufamasia lakini hajawahi kuajiriwa serikalini wala kwenye sekta binafsi.

Katika tukio lingine, mahakama ya Wilaya ya Ngara imemhukumu kifungo cha maisha gerezani, Ayubu John (20) kwa kosa la kumbaka mtoto wa dada yake mwenye miaka nane.

Malimi alisema Ayubu ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyakaribi wilayani Ngara alikamatwa na Polisi Oktoba 11, mwaka huu nyumbani kwake kwa kosa la kumbaka mtoto wa dada yake na kumfikisha katika mahakama ya Wilaya hiyo Oktoba 13, mwaka huu.

“Mtuhumiwa akiwa mahakani alikiri kosa la kumbaka mtoto huyo aliyekuwa anaishi naye nyumbani kwake kwa kumlazimisha jambo lililopelekea kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani,” alisema Malimi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles