24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

MFUMUKO WA BEI YA VINYWAJI WAPAA

Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sera kutoka NBS, Ephraim Kwesigabo

 

 

NA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

BEI ya bidhaa za vyakula na vinywaji baridi Aprili imeongezeka hadi kufikia asilimia 11.8 kutoka asilimia 11.0 Machi mwaka huu.

Hayo yalielezwa  jana na Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sera kutoka NBS, Ephraim Kwesigabo wakati akielezea mfumuko wa bei wa taifa kwa kipimo cha mwaka ambao unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Alisema mfumuko wa bei wa taifa wa Aprili mwaka huu  umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi uliopita.

“Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.04 kwa Aprili mwaka huu kutoka 102.46   Aprili mwaka jana,”alisema Kwesigabo.

Kwesigabo alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa   Aprili  mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 12.0 kutoka asilimia 11.7 ya  Machi mwaka huu.

Alisema badiliko la fahirisi za bei kwa bei kwa bidhaa zisizo za vyakula imepungua kidogo hadi asilimia 3.4  Aprili mwaka huu kutoka asilimia 3.6   Machi mwaka huu.

Alisema  mfumuko wa bei ambao hujumuisha vyakula na nishati kwa   Aprili mwaka huu, umeongezeka kidogo hadi asilimia 2.3 kutoka asilimia 2.2 ya  Machi mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles