33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Meya Tabora aonya watakaotumia vibaya fedha za Rais Samia

Na Allan Vicent, Tabora

MADIWANI na Watendaji wa Serikali mkoani Tabora wametakiwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia ipasavyo fedha zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

Hayo yamebainishwa jana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora, Ramadhan Kapela katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.

Alisema katika kipindi kifupi tu cha utawala wake, Rais Samia ametoa fedha nyingi sana kwa halmashauri hiyo ambazo hazikuwemo hata kwenye bajeti yao ya maendeleo, hivyo kuchochea kasi ya utekelezaji miradi mingi ya maendeleo.

Alisisitiza kuwa ni jukumu la madiwani na watendaji wa halmashauri ni kuhakikisha fedha hizo zinazitumika kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo, alionya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayezitumia vibaya.

“Rais Samia anafanya kazi kubwa sana, naomba tumuunge mkono kwa kusimamia ipasavyo miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za serikali ya awamu ya 6 zaidi ya Sh bilioni 1.5 tulizoletewa ili kazi iendelee kwa kasi kubwa,” amesema. 

Mstahiki Meya alibainisha kuwa kasi na utendaji wa Rais Samia unawarahisishia kazi Madiwani na Wabunge na kuongeza kuwa miradi inayotekelezwa kama itasimamiwa vizuri uchaguzi wa mwaka 2025 utakuwa mwepesi sana.

Aidha, katika kuhakikisha mabilioni hayo yaliyoletwa na Mheshimiwa Rais yanatumika ipasavyo aliomba Mkurugenzi Mtendaji wa Manispa hiyo, Dk. Peter Nyanja kuitisha kikao cha haraka cha madiwani, watendaji na wakuu wa shule ili kila mmoja awe makini na fedha hizo, wala asizichezee. 

Dk. Peter Nyanja alibainisha kuwa fedha zote zilizoletwa na Mheshimiwa Rais zitatumika ipasavyo kwa miradi iliyokusudiwa na hakuna hata senti moja itakayoibiwa, aliwataka Wakuu wa Idara wote kutokaa maofisini bali waende kufuatilia mapato na kuangalia miradi inayotekelezwa. 

Naye Mkuu wa wilaya ya Tabora, Dk. Yahaya Nawanda alisema haijawahi kutokea katika kipindi cha miezi 3 tu Rais amewaletea sh bil 1.5 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara na Sh bilioni 1 kwa ajili ya elimu, hili halijawahi kutokea.

Aliwataka madiwani kuhakikisha miradi yote ikiwemo ya elimu iliyotengewa fedha na kuanza kutekelezwa katika kata zao inasimamiwa ipasavyo ili kuwanufaisha wananchi, alisisitiza kuwa atakayekwamisha miradi hiyo hatafumbiwa macho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles