26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 59 zatumika kukopesha Vijana 33 Bodaboda Ngara

Na Allan Vicent, Ngara

KATIKA kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera imewezesha vijana wake 33 mikopo nafuu ya usafiri wa bodaboda yenye thamani ya zaidi ya sh mil 59.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Solomon Kimilike alipokuwa akiongea na Mtanzania Digital Ofisini kwake ambapo alieleza kuwa vijana hao wamewezeshwa kupitia vikundi vyao ili kuwainua kiuchumi.

Amesema mikopo hiyo ambayo inatokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri ni sehemu ya utekelezaji maelekezo ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambapo vijana wanapewa asilimia 4, wanawake 4 na walemavu 2.

“Tumekopesha vikundi 2 vya vijana vyenye jumla ya wanachama 33 jumla ya bodaboda 26 zenye thamani ya Sh milioni 59.8, na katika mwaka ujao wa fedha pia tutatoa bodaboda zingine kwa vikundi vya vijana kwa ajili ya mradi wao wa usafirishaji abiria,”amesema.

Mkurugenzi alifafanua kuwa kwa mwaka uliopita halmashauri yake ilitoa zaidi ya Sh milioni 169 ili kuwezesha wananchi kiuchumi ambapo jumla ya vikundi 13 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu vilinufaika.

Alibainisha kuwa kati ya vikundi 13 vilivyonufaika vya vijana vilikuwa 5, vya wanawake 5 na watu wenye ulemavu 3 ambapo aliyataka makundi yote kutumia mikopo hiyo vizuri na kwa kazi iliyokusudiwa na warejeshe kwa wakati.

Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri hiyo, Emanuel Kulwa amesema kuwa halmashauri imeongeza kazi ya ukusanyaji mapato kutoka katika vyanzo vyake vyote ili kuhakikisha vikundi vingi zaidi vinawezesha mikopo hiyo.

Alitaja vikundi vya vijana vilivyopatiwa mikopo ya bodaboda kuwa ni Twitezimbele na Mkombozi vilivyopo katika kata ya Ngara mjini na kuongeza kuwa vikundi vingine 3 vya vijana vilikopeshwa sh mil 48 kwa ajili ya miradi yao.

Viongozi wa Vikundi hivyo, Jafeti Makule (Twitezimbele) alisema kuwa mkopo huo umewainua sana vijana kwa kuwa sasa wana vipato vya uhakika na wengi wao wamejenga nyumba na kuoa wake.

Eustachius Laurant, Mwenyekiti wa kikundi cha Mkombozi alisema kuwa wamejiwekea utaratibu wa kurejesha kiasi cha Sh milioni 2.5 kila mwezi na ana uhakika ifikapo mwezi Juni mwakani watakuwa wamerejesha mkopo wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles