27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Meya Shinyanga afariki dunia

Na SAM BAHARI, SHINYANGA

 ALIYEKUWA Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mathew Nkulila, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga alikokuwa anafanyiwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa familia nyumbani kwa Nkulila ambaye ni  mjomba marehemu, Mary Joseph amesema marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa kipindi kirefu.

Mary amesema alianza kuugua Juni mwaka huu na kukimbizwa katika hospitali   Kamanga ya Mwanza ambako alilazwa na kupatiwa  matibabu.

Amesema baada ya kupata nafuu alirejea nyumbani kwake ambapo juzi alianza kuumwa tena na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa, Shinyanga na  saa 9.00 usiku alifariki dunia.

Mary amesema marehemu ameacha watoto wanne na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Jumatano wiki hii.

Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Ester Makune amesema Halmashauri ya imempoteza kiongozi muhimu mchapakazi na mpenda  maendeleo.

“Ndugu zangu wandishi, halmashauri yetu imempoteza kiongozi ambaye kwa kweli alikuwa dira ya maendeleo,mpenda haki,kimbilio la wanyonge, mbunifu na alitumia muda wake mwingi kuwatetea watu wenye kipato duni” amesema Ester.

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Mabambasi,Bakari Juma katika Kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga amesema kifo cha Nkulila ni pigo  kwani alikuwa mzaledo na chapakazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles