27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Messi, Ronaldo wamchanganya Pogba

downloadZURICH, USWISI

KIUNGO wa klabu ya Juventus na timu ya Taifa ya Ufaransa, Paul Pogba, amedai kwamba anatumia muda mwingi kwenye runinga kuangalia jinsi Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanavyocheza.

Mchezaji huyo amedai kwamba ndoto zake ni kuja kuwa mchezaji bora wa Ballon d’Or kama ilivyo kwa wachezaji hao na ndiyo maana Pogba anatumia muda mwingi kuwaangalia jinsi gani wanafanya wakiwa uwanjani.

“Natumia muda mwingi kwenye runinga kumwangalia Messi na Ronaldo kwa kile ambacho wanakifanya wakiwa uwanjani, hawa ni wachezaji ambao wapo kwenye uwezo wa hali ya juu kwa sasa.

“Wanashindana kuchukua tuzo ya Ballon d’Or na kuweka rekodi mbalimbali, lengo langu kubwa ni kucheza soka la kiwango cha juu ili niweze kufikia uwezo wa wachezaji hao au zaidi na ninaamini inawezekana kama nitajituma,” alisema Pogba.

Hata hivyo, mchezaji huyo amekanusha kwamba ana mpango wa kujiunga na klabu ya Barcelona katika kipindi hiki cha Januari.

“Sijawahi kusema kama nina mpango wa kujiunga na klabu ya Barcelona, kwa sasa akili yangu ni kuangalia jinsi gani ninaweza kuisaidia klabu yangu ya Juventus kwa kuwa nipo hapa,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles