24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Van Gaal awatupia lawama Lingard na Fellaini

Louis van GaalMANCHESTER, ENGLAND

BAADA ya klabu ya Manchester United kutoka sare ya 3-3 dhidi ya Newcastle United, kocha Van Gaal amewatupia lawama wachezaji wake, Jesse Lingard na Marouane Fellaini.

Mchezo huo wa Ligi Kuu nchini England ambao ulipigwa juzi kwenye Uwanja wa St. James Park, Manchester walishindwa kutamba mbele ya wenyeji wake japokuwa klabu hiyo ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-0.

Hata hivyo, Van Gaal aliwatupia lawama wachezaji wake kwa kupoteza nafasi ambazo walizipata katika mchezo huo.

“Tunaweza kujilaumu wenyewe kwa kuwa tulikuwa na uwezo wa kuumaliza mchezo mapema kutokana na jinsi tulivyokuwa tunaumiliki, lakini wachezaji wangu kama vile Jesse Lingard na Marouane Fellaini walipata nafasi za kutupatia furaha lakini walishindwa.

“Tumefanikiwa kupata mabao matatu na wao wamepata matatu lakini haina maana yoyote kwetu kwa kuwa tumeondoka na pointi moja wakati tulikuwa na nafasi ya kuondoka na pointi tatu.

Katika mchezo huo mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, alitoa mchango mkubwa wa kupachika mabao mawili katika sare hiyo ya mabao 3-3.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles