PARIS, Ufaransa
MPACHIKAJI mabao wa Kiargentina, Lionel Messi, ameibuka na kumshangaa Rais wa Barcelona, Joan Laporta, akisema bosi huyo alitaka abaki Catalunya ili acheze bila kulipwa.
Inafrahamika kuwa Barca walilazimika kumwacha Messi aende PSG kwa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi klabuni hapo na hilo liliambatana na kushindwa kusajili wachezaji wakubwa.
Messi alikubali kukatwa asilimia 50 ya mshahara wake lakini bado Barca hawakuweza kumudu kumlipa, jambo ambalo anaona Rais Laporta alitaka acheze bure.
“Sikuombwa kucheza bure. Niliombwa kukatwa asilimia 50 ya mshahara. Nilikubali bila tatizo lolote. Hivyo ndivyo nilivyotaka kuisaidia Barcelona…” amesema mshambuliaji huyo.