22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Meridian Bet, Lions Club zasaidia matibabu kwa walemavu wa macho 100

Waathirika 100 wenye ulemavu wa macho jijini Dar es Salaam, wamepatiwa huduma ya kupima, matibabu na vifaa tiba katika kambi maalumu ya kupima macho iliyofanyika jana kwenye kituo cha jumuiya ya maendeleo ya waisilamu wasioona
Tanzania (VIMDAT).

Kambi hiyo iliyolenga kupima macho, kutoa miwani na matibabu mengine ya macho kwa wenye ulemavu jijini Dar es Salaam iliratibiwa na klabu ya Lions kwa kushirikiana na kampuni ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet.

Mwenyekiti wa VIMDAT, Salim Luis Benedictor alisema kambi ya macho iliyofanyika

jana inawapa faraja ya waathirika ambao baadhi yao walipatiwa dawa, miwani na wengine kutakiwa kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuwasaidia kuona kidogo. Aman Maeda wa kitengo cha ustawi wa jamii wa Meridian Bet aliyeambatana na viongozi wengine wa kampuni hiyo alisema wameamua kushirikiana na klabu ya Lions ili kuigusa jamii hiyo.

“Kwetu kambi hii muhimu kwa kuwa inagusa mahitaji yao na wapo ambao watafanyiwa upasuaji mdogo, hivyo nitowe wito kwa jamii kuendelea kuwasaidia wenzetu hawa ili kupunguziwa makali ya tatizo linalowakabiri,” alisema.

Mratibu wa kambi hiyo kutoka Lions Club, Rizwan Qadri alisema watu 100 wameshiriki kwenye kambi hiyo ambayo ilianza kwa kuwapima na waliohitaji kupewa dawa au miwani walipatiwa.

“Waliobainika kuwa na matatizo makubwa zaidi tutawapeleka CCBRT na Muhimbili kwa mtibabu zaidi kwa kushirikiana na wenzetu wa Meridian Bet,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles