22.5 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Membe afariki dunia, Rais Samia amlilia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambae pia aliwahi kuwa  mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe amefariki dunia mapema leo Mei 12, 2023.

Membe amefariki dunia katika hospitali ya Kairuki iliyopo Mikocheni,jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya kifua.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na taarifa za kifo cha Membe ameandika kupitia Ukurasa wake rasmi wa twitter kuwa: “Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe. Kwa zaidi ya miaka 40 Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyetumikia nchi yetu kwa weledi.

“Pole kwa familia, ndugu, jamaa&marafiki. Mungu amweke mahali pema. Amina,” ameandika Rais Samia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles