22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimia 40 ya zao la dagaa linapotea-TAFIRI

*Mvua, masoko vyatajwa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI), Dk. Ismael Kimirei amesema asilimia 40 ya zao la dagaa linapotea.

Hayo amezungumza leo mEI 12, 2023 jijini Dar es Salaam kwenye kikao kilichowakutanisha wavuvi na wadau mbalimbali wakati wakitoa tathimini ya Utafiti waliofanya wa zao la dagaa amesema Lengo ni kupunguza uharibifu wa zao la dagaa.

“Utafiti huu umegawanyika sehemu kuu tatu Uvuvi, matunzo na uchakataji kila tani moja ya dagaa kilogramu 400 zinapotea kwa sababu mbalimbali na unasambaza vipi dagaa wakati asilimia 40 inapotea ,”amesema Dk. Kimirei.

Amesema kabla ya kufanya Utafiti huo waliofanya mafunzo katika utafiti huo wamewafikia wavuvi 619.

Amesema asilimia 42 ya samaki wanaovuliwa ni dagaa hivyoo zao la dagaa ni la mikakati kuongeza mazao yanayo safirishwa nje ya nchi.

Dk. Kimirei amesema changamoto kubwa kwa wavuvi ni utoaji taarifa ilikuwa tatizo wakijua wanataka kulipishwa kodi wakati wanafanya Utafiti.

Aidha, amesema Utafiti huo umetolewa ufanyike mabara matatu ikiwemo Afrika ikiwemo Tanzania.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, Stephen Lukanga amesema wadau mbalimbali wanatoa mapendekezo kudhibiti upotevu wa zao la dagaa.

Amesema asilimia kubwa ya zao la dagaa wanapotea wakati wa mvua na upande wa Masoko.

“Tulianza kufanya Utafiti mwaka juzi tuliwafikia wavuvi wa ziwa Tanganyika, Victoria, Nyasa na ukanda wa Pwani kutoa elimu kwa wavuvi, kuangalia miundombinu na kuwa na chombo bora,” amesema Lukanga.

Aidha, amesema Utafiti huo umedhaminiwa na Serikali ya Norway na Shirika la Kimataifa la Kilimo na Uvuvi .

Nae Katibu wa Mtandao wa Wanawake Wavuvi na Wachakataji wa Mazao ya Uvuvi (TAUFA), Hadija Malibiche amesema wamepokea vizuri utafiti na sekta hii wamepata ufumbuzi.

“Changamoto moto kubwa ni miundombinu na teknolojia kutengenezewa majiko ya kisasa na kuwawezesha kufanya biashara ya dagaa mipakani kwa sasa wafanyabiashara kuto nje wanafuta dagaa nchini wananunua kwa bei ndogo,”amesema khadija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles