30 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

MELI ZAGONGANA CHINA, 32 HAWAJULIKANI WALIKO

BEIJING, CHINA


WATU 32 hawajulikani waliko baada ya meli ya mafuta na ile ya mizigo kugongana mashariki mwa Pwani ya China juzi jioni.

Kwa mujibu wa taarifa, meli ya Sanchi yenye usajili wa Panama iliyokuwa imebeba tani 136,000 za mafuta, ambayo ilikuwa inatoka Iran, ilishika moto baada ya ajali hiyo.

Meli ya mizigo ya usaljili wa Hog Kong CF Crystal ilikuwa imebeba tani 64,000 za nafaka kutoka Marekani kwenda Guangdong, China.

Ajali hiyo ilitokea karibu kilomita 296 kutoka Pwani ya Shanghai.

Wizara ya Uchukuzi nchini China ilisema kuwa kati ya watu waliopotea kutokana na ajali hiyo, 30 walikuwa raia wa Iran na wawili wa Bangladesh.

Katika hatua nyingine, ilielezwa kuwa wahudumu 21 wa meli ya mizigo waliweza kuokolewa.

Picha iliyochapishwa na kituo cha taifa cha CGTN, ilionyesha moto mkubwa na moshi ukitoka kwenye meli ya mafuta.

Hata hivvyo, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Xinhua,  meli nane za China zimetimiwa kwa oparesheni ya uokoaji na tayari Korea Kusini nayo imetuma meli ya walinzi wa pwani na helikopta kusaidia zoezi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles