30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

AZAM FC YAWAZIA FAINALI MAPINDUZI CUP

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM


KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Iddy Cheche, amesema baada ya kufanikiwa kutinga  nusu fainali ya  michuano ya Kombe la Mapinduzi, wanajipanga kuhakikisha wanatinga fainali.

Azam juzi ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada  ya kuwanyuka Wekundu wa Msimbazi, Simba bao  1-0, mchezo uliopigwa Dimba la Amaan, Unguja.

Azam ipo kundi A katika michuano hiyo ikiwa pamoja na Simba, URA, Mwenge na Jamhuri.

Ilifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kufikisha  kushinda michezo yake mitatu na kufikisha pointi tisa, URA ikiwa katika nafasi ya pili na pointi saba, Simba kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne, Jamhuri kwenye nafasi ya tano ikiwa na pointi moja.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Cheche alisema  kikosi chake  kinazidi kuimarika siku baada ya siku, hatua inayomfanya aamini  kina fursa ya kutwaa taji hilo kwa mara nyingine.

“Baada ya kupata ushindi dhidi ya Simba, kwa sasa tunaendelea na mazoezi  lengo likiwa ni kuhakikisha tunajiweka imara kabla ya mchezo wa nusu fainali.

“Kusudio letu ni lile lile kuhakikisha tunatetea ubingwa wa michuano hii,”  alisema.

Cheche akiwa anakaimu nafasi ya kocha mkuu wa Azam, aliiongoza kutwaa ubingwa wa michuano iliyopita ya  Kombe la Mapinduzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles