21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mechi za AFCON kuibeba Yanga

PluijmNA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans van der Pluijm, amesema wachezaji waliokwenda kuzichezea timu zao za taifa wanapaswa kuelewa majukumu yao, ili waweze kunufaika na uzoefu wanaopata kwenye michuano ya Afrika.

Wachezaji 11 wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameitwa kuzichezea timu zao za taifa katika mechi za kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwaka 2017, nchini Gabon.

Yanga iliwahi kuwakatalia nyota wake walioitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, wakati ilipokuwa kambini Mbeya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema wachezaji 14 waliobaki wanaendelea na programu ya mazoezi anayowapa, huku wakisubiri kuungana na wenzao wiki ijayo, kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu inayoanza Septemba 12, mwaka huu.

Pluijm alisema hana wasiwasi kuwakosa wachezaji hao kwenye mazoezi yanayoendelea, kwani anaamini mbinu wanazopata kwenye timu zao za taifa watazifanyia kazi ili kutekeleza majukumu yao ndani ya Yanga.

“Hatuna shaka, tunachotakiwa kufanya ni kuwasubiri watimize majukumu kwenye mataifa yao na watakaporejea kikosini, naamini watakuwa wamejifunza mengi kutokana na mazoezi waliyopewa,” alisema,

Nyota wa Yanga waliopo Stars ni kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mwinyi Haji, Salum Telela, Simon Msuva, na Deus Kaseke.

Wachezaji wa kulipwa walioitwa kuzichezea timu zao ni kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, Mrundi Amissi Tambwe na Mtogo Vicent Bussou.

Stars inanolewa na Charles Boniface Mkwasa, ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga, jambo ambalo limemwondoa wasiwasi kocha huyo raia wa Uholanzi kutokana na kutambua mfumo na mbinu anazotumia kuwa zinaweza kuwasaidia wachezaji wake.

Pluijm, aliyeipa Yanga ubingwa wa msimu uliopita pamoja na Ngao ya Jamii, amepania kuanza vyema Ligi Kuu ili kukabiliana na ushindani uliopo na kutetea taji hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles