24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kanye West, Justin Timberlake wapondana

kanye_and_justin_timberlakeNEW YORK, Marekani

MSANII wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, amewaponda wasanii wenzake akidai wanakosa tuzo mbalimbali kutokana na kukosa heshima kwa wasanii wenzao.

Dongo hilo alilirusha kwa msanii wa RnB, Justin Timberlake, Ceelo Green na wasanii wengine, akidai ndiyo maana hana sababu ya kuhoji kwa nini wamekosa tuzo ya ‘MTV Video Music’.

“Nawachukia sana wasanii wasio na heshima kwa wasanii wenzao, akiwemo Timberlake, Ceelo Green na wengine wengi, ndiyo maana sishangai kuona wanakosa tuzo,” alisema Kanye West, akiwa amealikwa katika tuzo za MTV Video Music zilizofanyika nchini humo.

Hata hivyo, Timberlake alijibu maneno ya mwana hip hop huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter akidai mwana hip hop huyo ni mrembo.

“Kanye West ni msanii mrembo na hana uwezo wowote,” alisema Timberlake. Hata hivyo, msanii hiyo baadaye alionekana kukubali kauli ya Kanye West na kusema: “Nimeifuatilia vizuri kauli ya Kanye West na ninaamini yupo sahihi na ninamuunga mkono”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles